Na.WAMJW- DAR
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na
Ubunifu wa Uganda Dkt. Monica Musenero Masanza aliyeambatana na Wataalamu
kutoka Wizara hiyo ya Uganda.
Katika Mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika mapambano
dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 ili kulinda afya
za wananchi wa Tanzania na Uganda.
Aidha, Dkt. Gwajima amemhakikishia utayari wa Wizara yake kushirikiana na
Wizara yake nchini Uganda ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuleta
matokeo chanya katika Sekta ya Afya baina ya nchi hizo.
Naye Waziri wa Sayansi, Teknlojia na Ubunifu nchini Uganda Dkt. Monica
Musenero amesema, Uganda iko tayari kushirikiana na Tanzania katika katika
mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19.
Kikao hicho kimefanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment