Katika kuimarisha afya Kwa Wananchi wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Mkuu wa Wilaya hiyoo Hassan Masalla amewaomba wakazi wote wa wilaya hiyo na wilaya jirani kushiriki mbio za Jogging pamoja na mazoezi ya viungo.
DC Masalla ameyasema hayo Jumamosi Octoba 9, 2021 wakati wa ukimbiaji wa mbio za kilomita nane ambazo zimeanzia uwanja wa Sabasaba hadi mzunguko wa Malaika Hotel na kurudi uwanja wa sabasaba.
DC Masalla amesema toka waanzishe Ilemela Jogging Club mwezi wa tisa mwaka huu wamepata matokeo chanya kutokana na idadi ya washiriki na hii inatia moyo kuwa na ongezeko la washiriki Kila mwezi.
"Toka tuanzishe Ilemela Jogging Club mwezi uliopita, tumepata idadi Nzuri sana ya washiriki. Sisi kama Serikali ya Wilaya tunawapongeza washiriki wote waliojitokeza kuwaomba wengine wapya kuongezeka Kila mwezi mara tunafanya mazoezi mara moja Kwa mwezi" alisema DC Masalla.
Mheshimiwa Masalla amesema watu wakijali mazoezi magonjwa nyemelezi huwa yanaondoka maana Mwili unakuwa na kinga ya kupambana na magonjwa, kama agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi kila mara.
Pia DC Masalla amewaomba washiriki wa Jogging wale ambao hawajapata Chanjo ya Covid 19, kuwa Chanjo ipo vituo vyote vya afya Wilaya ya Ilemela hivyo Kwa hiari yao wakapime na kupata Chanjo Ili kujilinda na ugonjwa wa Corona.
Post a Comment