Naibu Mkurungenzi wa Halopesa Magesa Wandwi,Afisa Mahusinao ya nje Yassir
Matsawily (katikati) wakiwa pamoja na Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Masoko
Sakina Makabu (wa kwanza kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo wakikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya Kijamii kwa Afisa
mahusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili Patric Mvungi ( wa pili
kulia) na baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo
walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili
(MOI) na kuwapelekea mahitaji hayo ikiwa ni katika kuadhimisha miaka sita ya
utoaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Mawasiliano Halotel Pamoja na baadhi
wa maofisa wa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) wakiwa katika picha
ya pamoja wakati wakikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii leo
wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji hayo
ikiwa ni katika kuadhimisha miaka sita ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa
nchini.
Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Masoko Sakina Makabu akiongea na waandishi
wa habari leo, baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii kwa
watoto na wazazi walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili wakati
wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea na kuwapelekea mahitaji hayo ikiwa
ni katika kuadhimisha miaka sita ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa
nchini.
Afisa Mahusiano ya nje wa Halotel Yassir Matsawily akiongea na waandishi
wa habari leo, baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya
kijamii kwa watoto na wazazi walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea na
kuwapelekea mahitaji hayo ikiwa ni katika kuadhimisha miaka sita ya utoaji wa
huduma za mawasiliano hapa nchini.
NA
MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Katika
kuonyesha thamani na kujali jamii kwenye Sekta ya Afya na elimu,Kampuni ya simu
ya Halotel imetoa mahitaji muhimu kwa watoto wenye changamoto ya kiafya ya
vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa
Muhimbili (MOI) yatakayowawezesha kuimarisha afya zao.
Hayo
yamejiri leo jijini Dar es salaam katika kuadhimisha miaka 6 ya kampuni hiyo na
utoaji wa huduma ya mawasiliano ambapo wameadhimisha kwa kwa utoajni wa Dawa
muhimu ya kibinadamu ili kuwasaidia afya zao pindi wawapo wodini wakisubiri
kupatiwa matibabu kwa njia ya upasuaji.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mahitaji hao,Afisa Uhusiano wa Nje Halotel Yassir Matsawily
amesema katika kuhakikisha wanasaidia sekta afya wametumai fursa hiyo
kuwatembelea watoto hao kwa kusheherekea na kuwapa misaada ili waweze kuimarika
kiafya.
‘Hii
imekuwa kawaida yetu kwa kutoa kidogo tulichojaaliwa kwa wnzetu katiika jamii kwani lengo letu ni
kuonyesha upendo kwao na kutambua thamani yao katika jamii ya watanzania’amesema
Yassir
Kwa
upande wake Msemaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Patrick Mvungi
ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuguswa na kutoa msaada wao kwa jamii huku
akiyataka makampuni mengine kuiga mfano kwani wanawasaidia wagonjwa kupata
faraja.
‘Hii
ni hatua mpya na kubwa kwani imekuwa endelevu kwetu sisi katika kuimarisha
ushirikiano wetu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekta ya
afya kwa ujumla’amesema Mvungi
Mmoja wa wazazi Bi Rose Vincent akizungumza
kwa niaba ya wazazi wenzake baada ya kukabidhiwa msaada huo wameiomba Kampuni
hiyo kuendelea kuwa kuonyesha mchango wao kwa jamii kwani wanawasaidia
watanzania wote wenye uhitaji walio katika vituo vya afya.
Hata hivyo Kampuni hiyo imesema huo ni muendelezo wa kuendelea kutoa mchango wao kwa jamii ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuboresha huduma za afya.
Post a Comment