Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Julius Wambogo (picha na maktaba)
NA
MUSSA KHALID,
Jukwaa
la Huduma kwa njia ya Mtandao la Mchongo limepanga kuwaunganisha wafanyabishara
na mashirika mbalimbali nchini katika kuwasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Julius Wambogo amesema wameamua kutumia njia
teknolojia ya kidigitali kutokana na kuwa ni njia mpya mpya kwa sasa
inayosaidia watu kujipatia huduma mbalimbali.
Wambogo
amesema kuwa kupitia Jukwaa hilo la Mchongo wamekuja na utatuzi wa changamoto
mbalimbali kwa wafanyabiashara na makampuni mbalimbali kwa kutoa eneo ambalo
wabunifu na watu wanaweza kuonyesha ujuzi wao na hivyo kupata urahisi katika
makampuni yao.
‘Tanzania
tuna takriban Mill watu 58 na wahitimu wa vyuo kila mwaka ni zaidi ya watu 1000
na tukiangalia uhalisia wahitimu hawa ni wachache wanapata ajira wengi wao
huingia mitaani na kuanza kufanya biashara ndogondogo wengine hawana cha
kufanya lakini kumbe kuna namna nyingi ambayo wangeweza kuonyesha ujuzi
wao,uwezo wao na kipaji chao’amesema Wambogo
Aidha
Wambogo ameeleza kuwa Jukwaa hilo linasaidia pia watu kijipatia huduma
mbalimbali sambamba na kuongeza elimu ya watu kuwa na nidhamu kwenye kazi
pamoja na bidii.
Amesema
kwa sasa Jukwa hilo lipo wazi kwa watumiaji kwani umeundwa kwa ajili ya watu wa
aina zote wakiwemo watu wa kwenye Makampuni,,walemavu,watu wa kwenye mataasisi
ndani na nje ya nchi na wenye ujuzi na ubunifu kwenye sekta mbalimbali kwani
lengo lao ni kuweka urahisi wa kutafuta watu wakati wowote.
‘Ili
kusaidia ukuaji na uendeshaji wa Mchongo tunatazamia kushirikiana na mataasisi
ya sekta binafsi na mashirika ya wizara za Tanzania na biashara za ndani na njea ya nchi ambayo
ina ndoto na mpango wa kuongeza kipato chao na ubunifu wao ili kukuza ukuaji
endelevu wa kiuchumi na kumaliza umaskini Afria’ameendelea kusema Wambogo
Hata
hivyo amesema wanatarajia kujnga uchumi wa kijamii na wa taifa la Tanzania kwa
kutoa njia rahisi za kazi kwenye dimbwi moja la watu wenye ubunifu kwa bajeti
ya kuendesha miradi kwa bei nafuu kwa watoa huduma ili kujenga kile
kilichoathiriwa na changamoto mbalimbali.
Post a Comment