**********************************
Msanii anaetumia kipaji chake cha kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine Ikuzi Kicheko, 'Mzalendo halisi' amezindua kampeni ya Natembea na mama Kazi iendelee.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar es Salaam, amesema kampeni hiyo ni ya kumuunga mama mkono ambapo watatembea na mama.
"Natembea na Mama Kazi iendelee Mguu kwa mguu, chocho kwa chocho kwa maendeleo ya Taifa letu, tutaanza Oktoba 23 Rufiji, Dar es Salaam hadi Oktoba 29 Zanzibar.
Aidha amesema kuwa matembezi hayo yatagusa elimu afya na kuangalia miundombinu mbalimbali iliyotengenezwa na serikali na kuweza kusaidia dawa kwenye hospital na mashule mbalimbali.
"Tunahitaji bidhaa kama nguo, madaftari, vifaa mbalimbali vitakavyoweza kuwasaidia watu kwenye huitaji ili kuwapa faraja kwa njia Mona hama nyingine tutaweza kufikisha kwa wahusika."amesema Kicheko
Kwa upande wa Makumbusho ya Taifa wamesema kuwa dhamana yetu nikutumia kijiji cha makumbusho kupeleka ujumbe katika jamii nzima juu ya uzalendo.
Post a Comment