Mkurugenzi Mtendaji qa TASAF Ladislaus Mwamange akizungumza
na waandishi wa habari hawapo pichani akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo kwa Ustawi wa taarifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.
............................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Imeelezwa kuwa kiasi cha fedha Sh.Bil 5.5 zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF zitaelekezwa katika utoaji wa Ruzuku na utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa kaya za walengwa ili kupata kipato kitakachoziwezesha kaya hizo kujikwamua kiuchumi na kupunguza athari za UVIKO 19.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji qa TASAF Ladislaus Mwamange wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa taarifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa mpango wa kunusuru Kaya za walengwa wa TASAF.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia fedha Hizo kaya za walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wanaoishi katika maeneo ya Mijini,watafanyakazi katika miradi ya Jamii na Kulipwa ujira wa wastani wa Sh.135,000 kwa kila kaya ili kufufua na kuimarisha shughuli zao.
"TASAF itazitumia fedha Hizo kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mlipuko wa UVIKO -19 kwa kaya za walengwa wa TASAF ambao serikali imedhamiria kuwaondoa katika umaskini wa kipato kwa kuwapatia Ruzuku za kujikimu,ajira
Aidha Mwamange amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali katika kupunguza umaskini wa watanzania wanaoishi kwenye mazingira duni na inafanta jitihada kubwa kupata fedha kutoka vyanzo vya ndani.
"Utoaji wa sehemu ya Mkopo huu nafuu kwa ajili ya mpango wa TASAF ni kielelezo tosha kwamba serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi wake hasa wale wanaoishi katika mazingira duni"amesema Mwamange
Vilevile Mwamange amesema Menejimenti ya TASAF kwa mwongozo wa Kamati ya Uongozi ya Taifa itahakikisha maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa walengwa katika maeneo yatakayoanishwa unaanza mara tu baada ya fedha Hizo kupokelewa.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo amemuhakikishia Rais Samia kuwa utekelezaji wa miradi mbalimbali utafanywa kwa wakati na hakuna hakuna fedha ambazo zitatumika Nje ya Malengo yaliyokusuduwa.
TASAF inatekeleza
mpango wa kunusuru kaya masikini katika halmashauri 184 za Tanzania Bara, Unguja,
na Pemba ambapo idadi ya walengwa ni
kaya milioni 1.4 zenye watu wanaokadiriwa kufikia milioni 10.
Post a Comment