MAMBO NA VIJAMBO KUFANYA VICHEKESHO VYA JUKWAANI LEO




*************************************

Na Mwandishi wetu


Kikundi cha uchekeshaji cha Mambo na vijambo inatarajia kufanya show ya standup Comedy kesho 29 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mmoja ya wachekeshaji wa kundi hilo la Mambo na Vijambo, Ayubu mzee wa 'Yanini tupike miogo kwenye shughuli ya harusi', amesema kuwa awali walizoea kuandaa maigizo ya kwenye televishioni lakini sasa wanafanya na vichekesho vya jukwaani.


"Tunawaomba wa Tanzania kujitokeza kwa wingi waje washuhudie tukichekesha tunaweza kusema stress free njoo tuzikamue strees tukianika mwezi Novemba kichwa kisiwe na mawazo yoyote" amesema Ayubu


Kwa upande wake Rais wa Shirikisho LA Filamu, Elia Mjata amesema kuwa ni wakati wa burudani za kutosha hivyo wapenda vichekesho wajitokeze kwa wingi kuweza kupunguza mawazo.


"Kutakuwa na burudani za kutosha pamoja na dance kutoka kwa vijana wa kihindi na watacheza na baadae tutaendelea na vichekesho vya jukwaani usipange kukosa wote mnakaribishwa" amesema Mjata

0/Post a Comment/Comments