MAWAZIRI WANNE SUDAN WAKAMATWA NA JESHI


Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu wa sudan na kote nchini humo


Wanajeshi wamevamia nyumbani kwa mshauri wa habari wa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok na kumkamata mapema leo.

Televisheni ya Al hadath imesema wanajeshi wa Sudan wasiotambulika waliwakamata mawaziri wanne wa serikali na raia mmoja mwanachama wa baraza kuu la serikali.

Duru zinasema kuwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani.

Haya yalijiri siku moja tu baada ya Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Pembe wa Afrika Jeffrey Feltman kukutana na viongozi wa kijeshi na kiraia mjini Khartoum kutafuta mwafaka katika mzozo huo.

Source:DW

0/Post a Comment/Comments