Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Agness Kijazi akizungumza na waandishi wa habari kueleza utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.
..........................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuendelea kutoa taarifa za Hali ya Hewa ambazo
zinasaidia katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya usafirishaji wa ardhini na
majini pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya kimaendeleo.
Mhandisi
Kasekenya ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye
Mkutano wa 14 wa sekta ya Uchukuzi wenye lengo la kupima utendaji wa sekta
mbalimbali za uchukuzi.
Naibu Waziri Mhandisi
Kasekenya amesema Taasisi hiyo ni muhimu kwani inasaidia sekta zote katika
utekelezaji wa miradi ya kimkakati hususani ya barabara kufahamu taarifa za
hali ya hewa kwa yanayotarajiwa kutokea na kwa wakati gani.
Aidha Mhandisi Kasekenya amesema ni vyema katika ujenzi wa miradi yeyote kuhakikisha
unafatwa utaratibu wa kitaalamu wa kufahamu mazingira hayo ili kuweza kuepukana
na madhara yanayoweza kujitokeza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt
Agness Kijazi amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikitumika kwenye miradi mbalimbali
ya maendeleo kwenye sekta ya uchukuzi ikiwemo Anga,kwenye Reli,masuala ya barabara,na
miradi mikubwa ya ujenzi hata bwawa la Nyerere ambalo linaendelea na ujenzi.
‘Sisi
tupo hapa kuwaonyesha ni huduma gani tunazozitoa na kuwaonyesha jinsi tunatoa
utabiri na namna unavyotumika kwani ni muhimu katika sekta hizo na hasa katika
kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya tabia ya nchi DUNIANI hivyo tunawaeleza
wanavyoweza kuzitumia tabiri tunazozitoa katika shughuli zao’amesema Dkt Kijazi
Hata
hivyo Dkt Kijazi ameziasa taasisi mbalimbali kuangalia masuala ya hali ya hewa
ili kuepukana na kuweka mradi mikubwa kisha baadae likaja janga moja kubwa na kuufuta na
kujikuta unanza upya.
Mkutao huo 14 wa sekta ya Uchukuzi umezishirikisha taasisi mbalimbali za kiserikali zikiwemo za usafirishaji wa Ardhini na Majini kwa malengo ya kujadili utendaji kazi wa taasisi hizo katika ufanyaji wa shughuli zao.
Post a Comment