Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mtendaji wa
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa mitaji ya maendeleo (UNSDF) Bi. Preeti Sinha Ikulu
Jijini Dar es Salaam leo tarehe 25 Oktoba, 2021.
..........................................
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 25
Oktoba, 2021 amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa
Mataifa wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) Bi. Preeti Sinha, Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,imesema
Katika mazungumzo hayo, Bi Sinha amemueleza Mhe. Rais Samia kuwa UNCDF ipo
tayari kushirikiana na nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Serikali ya
Tanzania kutafuta njia mbadala za kupata fedha za kugharamia miradi ya
maendeleo.
Bi
Sinha amesema kupitia Mradi wao ujulikanao kama Municipal Investment Financing, unaweza kusaidia upatikanaji wa
fedha kwa Serikali za Mitaa kupitia uanzishwaji wa Hati Fungani
Fedha
zitakazo patikana kupitia Hati Fungani zitarejeshwa kutokana na makusanyo
yanayopatikana kwenye Serikali za Mitaa
Kwa
upande wake Mhe. Rais Samia amekubaliana na wazo hilo na kusema kuwa litasaidia
kupunguza mzigo kwa Serikali Kuu kuhudumia miradi ya maendeleo ya Serikali za Mitaa.
Mhe. Rais Samia ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kufanya uratibu utakaowezesha mpango huo kuanza kutekelezwa mara moja.
Post a Comment