MILIONI 315 KUING'ARISHA KATA YA KAWEKAMO KIMAENDELEO

 






Jumla ya shilingi milioni 315 zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Kawekamo Jimbo la Ilemela


Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika viwanja vya soko la zamani la Msumbiji ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kata kwa kata kusikiliza kero za wananchi, kuwashukuru Kwa kukichagua Chama Cha Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu uliopita na kutoa mrejesho wa vikao vya Bunge la bajeti 


Dkt Mabula  amewataka wananchi wa kata ya Kawekamo kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Kwa namna anavyojali watu wake Kwa kutoa fedha zitakazochochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa katika shule za msingi za Kilimani na Pasiansi utakaogharimu shilingi milioni 30, Milioni 51 kwaajili ya shule za sekondari za kata hiyo, kuongezwa kwa bajeti ya Barabara ndani ya Jimbo hilo kutoka Bilioni 1.2 hadi kufikia Bilioni 3.2, Kiasi cha shilingi Milioni 600 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya na Bilioni 1 kwaajili ya ujenzi wa barabara fedha zilizotolewa kwa kila Jimbo nchini


'.. Mara nyingi mwanamke akiwa kiongozi anajua namna ya kulea familia, Hata kina baba wanajua yeye anaacha mia Tano Ila anakuta Kila Kitu kipo sawa na Wala haulizi mama amefanyaje kufanikisha, anakula analala, Mipango ya Mama Rais Mhe Samia imejielekeza kusaidia mwananchi mmoja mmoja, Nani kama Mama ..' Alisema


Aidha Mhe Dkt Mabula akawataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kumuombea Rais Samia sanjari na kuwasisitiza kuhakikisha wanakuwa na Miliki za ardhi yao pamoja na kulipa Kodi za pango la ardhi


Kwa upande wake Afisa Tarafa wa wilaya ya Ilemela Ndugu Godfrey Mzava mbali na kumpongeza Mbunge huyo Kwa ukaribu wake na wananchi anaowaongoza akamhakikishia usalama na amani ndani ya Jimbo hilo pamoja na kuwataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 ikiwemo kujitokeza kupata chanjo Kwa hiari bila gharama yeyote inayotelewa maeneo yote ya huduma za afya



Nae mwakilishi wa mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni Afisa Ardhi na Mipango Miji Ndugu Shukran Kyando akawataka wananchi kufuata sheria za ardhi na mipango miji ikiwemo kuacha kununua ardhi kiholela bila kushirikisha wataalamu wa Manispaa ya Ilemela


Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula mbali na kumpongeza Mhe Rais Samia na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Kwa namna wanavyoshirikiana katika kuwaleta maendeleo wananchi akafafanua kuwa Ilani ya uchaguzi inatekelezwa vizuri ndani ya Jimbo hilo kwani vikao na maelekezo ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizoainishwa na Ilani zinafanyika kikamilifu


Akihitimisha Diwani wa kata ya Kawekamo Mhe Omary amemshukuru  Bunge wa Jimbo la Ilemela Kwa kufika ndani ya kata yake kuchochea utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na Rais Kwa kutoa fedha zitakazobadilisha kata yake huku akiwaomba wananchi kuuungana pamoja na kusukuma gurudumu la maendeleo

0/Post a Comment/Comments