POLISI DAR YAKAMATA WATUHUMIWA 76 WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU.

Kamanda wa polisi Kanda maalum Dar es salaam Muliro Muliro

.......................................... 

NA MUSSA KHALID 

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 76 kwa kujihusisha na makosa ya kijinai ambayo ni kero kwa wananchi wa Dar es salaam. 

Akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya habari Kamanda wa polisi Kanda maalum Dar es salaam Muliro Muliro amesema hiyo imetokana na muendelezo na jitihada za kuzuia uhalifu sambamba na kufanya misako mikali ya kuwafuatilia wahalifu mbalimbali wa makosa ya jinai katika jiji hilo. 

Kamanda Muliro amesema Miongoni mwa waliokamatwa ni wahalifu wanaojihusisha na wizi wa magari na vifaa vya kwenye magari ,wizi wa pikipiki, ukwapuaji wa mikoba kwa kutumia pikipiki, unyang’anyi wa kutumia silaha na matukio ya uvunjaji nyakati za usiku na mchana. 

Aidha Kamanda Muliro amesema kufuatia msako ambao umefanywa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ya jiji kuanzia tarehe Septemba Mosi mpaka Sept 30 mwaka huu wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 40 wanaojihusisha na makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha,uvunjaji wa nyumba nyakati za usiku na mchana,waporaji wa mikoba kwa kutumia pikipiki(vishandu). 

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kupitia mifumo ya kisheria kuanzia mwezi Januari 2021 hadi Septemba 2021 limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai na kupata mafanikio ya adhabu. 

Jumla ya kesi 08 za kubaka zilifikishwa mahakamani na watuhumiwa 08walikutwa na hatia na kupewa adhabu kama ifuatavyo:- Kifungo cha maisha ni watu 03, kwenda jela miaka 30 watu 03 na wengine wawili walihukumiwa miaka 20 kwenda jela. 

Jumla ya kesi 19 za unyang’anyi wa kutumia silaha zilifikishwa mahakamani na watuhumiwa 33 walikutwa na hatia na walihukumiwa kwenda jela miaka 30 jela. 

Jumla ya kesi 02 za kuvunja nyumba usiku/mchana na kuiba zilifikishwamahakamani ambapo watuhumiwa 04 walihukumiwa vifungo, 02 kati yao walifungwa miezi sita jela na 02 walifungwa miaka mitatu jela. 

Jumla ya kesi 05 za makosa ya kulawiti zilifikishwa mahakamani nawatuhumiwa 05 walifungwa, 02 kati yao walifungwa mwaka mmoja na kulipa faini huku watuhumiwa 02 walifungwa miaka 30, mtuhumiwa mmoja alifungwa kifungo cha nje na kulipa faini. 

Hata hivyo Kamanda Muliro amewataka wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano kwa Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wahalifu pindi watakapowabaini katika maeneo yao.

0/Post a Comment/Comments