RAIS SAMIA ATAJA MAMBO SITA YALIYOIPANDISHA UWEKEZAJI NCHINI KWA MIEZI SITA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametaja mambo sita yaliyochangia nchi kupata mafanikio katika eneo la uwekezaji tangu Mwezi Machi hadi Agosti, 2021. 


Mhe Rais ameyataja masuala hayo kuwa ni; Kuondolewa  kwa urasimu wa utoaji vibali vya kazi, Uanzishwaji wa Dirisha moja la kieletroniki la uwekezaji, Kanzi Data ya ardhi, Kituo cha Mawasiliano cha masuala ya uwekezaji, Uboreshaji wa majadiliano na sekta binafsi pamoja na ongezeko la usajili  wa  miradi ya uwekezaji.


Mhe. Rais Samia ameyasema hayo leo tarehe 10 Oktoba, 2021, Jijini Dodoma, wakati akizindua Kampeni ya Maendeleao kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19, ambapo amefafanua kuwa kutokana na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara nchini, hali ya uwekezaji imeongezeka ikilinganishwa na  hali  ya uwekezaji katika    kipindi kama  hicho  kwa mwaka jana .


 Mhe.ameyataja mambo yaliyofanywa na serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara, kuwa ni Kuondoa urasimu wa utoaji wa vibali vya kazi kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki ambao umepunguza muda wa kutoa vibali kutoka zaidi ya siku 14 za awali  hadi siku 1 au 3  kwa sasa ikiwa mwombaji ametimiza taratibu zote.


Hatua nyingine ambazo serikali imefanya ni kukamilisha Dirisha moja la kieletroniki la Uwekezaji, Kituo cha Mawasiliano cha masuala ya Uwekezaji, Kanzidata ya Ardhi yenye ukubwa wa hekta 1.6 milioni, Uimarishaji wa majadiliano na Sekta Binafsi, kwa kufanya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara.


Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa kutokana na hatua hizo miradi yenye thamani ya Dola za marekani bilioni 3.5 imesajiliwa ambayo inatarajia kuzalisha ajira 43,782, hivyo itasaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.


Miradi 164 yenye thamani ya Dola za marekani bilioni 3,158 imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Miradi 18 imeasjiliwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa uwekezaji Tanzani (EPZA) daola za marekani ikilinganishwa na kwa kipindi kama hicho  mwaka jana   ilisajiliwa miradi yenye thamani ya Dola za marekani milionii  647.43.


Katika hatua nyingine Mhe. Rais Samia amesema kuwa ukamilishwaji wa Filamu ya Royal Tour, ambayo anahusika katika kuitengeneza, ikikamilika na kutangazwa itawezesha kutangaza vivutio vya utalii na uwekezaji hivyo uwekezaji utaendelea kukua.


Mhe. Rais kwa mamlaka aliyonayo chini ya Ibara ya 36 (1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, aliunda Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, kama ilivyotangazwa katika Tangazo la Serikali Na. 384 la tarehe 07 Mei, 2021 na kupewa majukumu kupitia Tangazo la Serikali Na,534 la tarehe 02 Julai, 2021.

 

Ofisi ya Waziri Mkuu – uwekezaji, inaendelea kutekeleza majukumu ya uratibu wa Uwekezaji nchini, kwa mujibu wa Sera ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997, ambazo kwa pamoja na mambo mengine zimetoa mfumo wa kuratibu masuala ya uwekezaji nchini.

 

MWISHO.

0/Post a Comment/Comments