Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa onyo kwa
Wafanyabiashara wanaoendelea kufanya Biashara pembezoni mwa Barabara ya Airport
licha ya Vibanda vyao kuondolewa kuhama Mara moja na kwenda kwenye maeneo
yaliyotengwa.
RC Makalla ametoa onyo hilo mapema leo alipotembea mguu kwa mguu
kutoka Airport Hadi Chang'ombe kuona utekelezaji wa maelekezo ya Serikali
ambapo ameshuhudia baadha ya Wafanyabiashara wakijiiba na kupika vyakula chini
ya miti na kuwataka waondoke na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.
Aidha RC Makalla amesema kuvunja kibanda na kuendelea kupika Chini
ni kazi bure hivyo amewaelekeza Wakurugenzi,Watendaji wa Kata na Mitaa
kuhakikisha wanasimamia Wafanyabiashara hao wasirudi upya.
Hata hivyo RC Makalla amesema kwa unyeti wa Barabara ya Airport
atahakikisha anasimamia Barabara hiyo iwe na mandhari nzuri.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema zoezi hilo ni endelevu na
ifikapo November 06 Mkoa utazindua kampeni ya Usafi wa mazingira hivyo amewataka
Wenye ndoto ya kurudi kwenye maeneo yaliyokatazwa wasahau suala hilo.
Post a Comment