Mamia ya Wananchi na *wapenzi wa Burudani* wamefurika kwa wingi kwenye Tamasha kubwa la Burudani la *DAR SUNSET CARNIVAL* Coco Beach ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amesema Tamasha hilo litazinduliwa rasmi na *Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa*.
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo *RC Makalla* ametangaza kuwa *siku ya uzinduzi* rasmi kutakuwa na *Surprise nyingi za Burudani* hivyo amewataka *Wananchi kukaa mkao wa kula.*
Aidha *RC Makalla* amesema *tukio la leo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa* Kutokana na ubunifu wa *Maandalizi na mwamko mkubwa* wa Wananchi waliojitokeza.
Hata hivyo *RC Makalla* amesema *Maboresho ya ufukwe* wa Coco umewezesha kuwa na uwezo wa kuchukuwa zaidi ya *Wafanyabiashara 600 kutoka 200 waliokuwepo* ambapo amebainisha kuwa lengo la Serikali ni *kukuza utali wa fukwe kupitia fukwe zote za Mkoa huo.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* amepongeza *Kampuni zote zilizokubali kushirikiana na Serikali kujenga Vibanda vya kisasa bure* na kusema matatajio ni kuona wiki ijayo Ujenzi wa Vibanda vyote vinakamilika.
Maboresho ya ufukwe wa Coco Beach imejumuisha *Usafi wa fukwe, Ujenzi wa Vibanda vya kisasa, Ujenzi wa vyoo, Miundombinu ya Maji, Umeme na kuhakikisha huduma zote za Kifedha zinapatikana eneo Hilo.*
Post a Comment