- Atoa *Wiki moja kwa Wakurugenzi kuhakikisha Usafi wa kina unafanyika.*
- Awataka Machinga waliobomoa Vibanda na *kumwaga bidhaa Chini kuyaachia maeneo.*
- Asema *zoezi la kuwapanga linakwenda vizuri na ushirikiano ni mkubwa.*
- *Mji umeanza kuwa na mandhari nzuri.*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewaelekeza *Wakurugenzi wa Halmashauri, Watendaji wa Kata na Mitaa* kuhakikisha maeneo yote waliyoondoka Machinga yanafanyiwa *Usafi* na kuweka uangalizi wa kutosha ili *yasivamiwe upya.*
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao na Watendaji kata na Mitaa kuhusu *tathimini ya zoezi la kuwapanga Machinga* ambapo amesema *Zoezi Hilo linakwenda vizuri* kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Aidha *RC Makalla* amezitaka Halmashauri za Dar es salaam kuzitumia *kampuni Zilizopewa kazi ya Usafi* kwenye maeneo husika kutekeleza zoezi hilo la Usafi ndani ya *wiki moja.*
Kuhusu Wafanyabiashara waliokubali *kuvunja Vibanda* na Sasa *wanapanga bidhaa zao Chini kwenye* maeneo yaleyale yaliyokatazwa *RC Makalla* amepiga marufuku utaratibu huo na kuwataka *kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* amezielekeza *Taasisi zote za Umma* ikiwemo *Shule, Vyuo, Mashirika, Hospital* na nyinginezo kuhakikisha *hawaruhusu Wafanyabiashara kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa* huku akiwaelekeza *TANROAD na TARURA* kuzilinda Barabara zao *zisivamiwe upya.*
Sanjari na hayo *RC Makalla* amesema ifikapo *October 30 asionekane Mfanyabiashara yoyote akiendesha biashara Kwenye maeneo yaliyokatazwa* hivyo amewataka kutumia *muda wa nyongeza* uliotolewa kuhama.
Post a Comment