RC MAKALLA AWAELEZA MAKAMANDA WA CHUO CHA KIJESHI KUWA DSM INA VIWANDA VINGI NA SHUGHULI ZA KIUCHUM



- Ampongeza *Rais Samia Suluhu Hasan* kwa hatua alizochukua katika *kipindi Cha miezi 6 kukuza uchumi, kuvutia watalii Na Wawekezaji* na utalekelezaji wa *Miradi mingi ya maendeleo*.


- *Makamanda waridhishwa* na hatua za Serikali kuvutia wawekezaji kwa *kupunguza tozo, Mamlaka za udhibiti* kuwa sehemu moja na utekelezaji wa *Blue Print.*


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* leo ametembelewa na ugeni wa *makamanda* wa Kijeshi kutoka *Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu CSC Duluti* Cha Mkoani Arusha waliokuja Dar es salaam kwa ziara ya kujifunza Masuala ya *uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo endelevu.*


Ugeni huo unajumuisha *makamanda* wa Vyeo vya juu vya  Kijeshi kutoka *mataifa mbalimbali* ikiwemo *Misri, Burundi, Malawi, Zimbabwe,Kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania*.


Akizungumza na Makamanda hao, *RC Makalla* ametumia nafasi hiyo kueleza *jitiada* mbalimbali zinazofanywa na *Serikali ya awamu ya sita* Katika kuboresha na kuweka mazingira Bora ya *Uwekezaji na biashara* ikiwemo uanzishwaji wa *one stop Center ya Biashara* ya Mkoa huo ambayo inakwenda *kupunguza Urasimu.*


Aidha *RC Makalla* amewapongeza Makamanda hao kwa *uamuzi sahihi* wa kuchagua Mkoa wa Dar es salaam Kama sehemu ya *mafunzo* na amewahakikishia *usalama na ushirikiano* kwa muda wote watakaokuwepo Dar es salaam.


Ugeni wa makamanda hao unaongozwa na *Brigedia Jenerali Sylvester Damian Ghuliku* ambae ni Mkuu wa *chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Duluti* Cha Mkoani Arusha na watatembelea maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

0/Post a Comment/Comments