RC MAKALLA AWAPONGEZA DAWASA KWA UTATUZI WA KERO ZA MAJI MAENEO YA PEMBEZONI MWA DSM



Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* leo ametembelea na kukagua *Shehena ya Vifaa* vya kufikisha huduma ya maji kwa Wananchi ambapo ameonyesha *kuridhishwa na jitiada za DAWASA Katika kushughulikia tatizo la upatikanaji wa maji Dar es salaam.*


*RC Makalla* amesema hayo wakati wa ziara kwenye *bohari ya Vifaa ya DAWASA* ambapo pia amekabidhi hundi ya Shilingi *Milioni 232* kwa wakazi 7 wa eneo la *Mshikamano* waliokubali kuacha maeneo yao kupisha Mradi wa *Ujenzi wa Tank la Maji Mshikamano.*


Akizungumza kuhusu Mradi huo ambao unagharimu kiasi Cha *Shilingi bilioni 5.4, RC Makalla* amewahakikishia Wananchi wa *Jimbo la Kibamba* kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutaoa Fursa kwa kila mwananchi kupata *huduma ya maji Safi na Salama.*


Aidha *RC Makalla* amepongeza jitiada za Serikali ya awamu ya sita Chini ya *Rais Samia Suluhu Hassan* Katika kushughulikia na kupatia ufumbuzi *kero ya Maji* ambapo amesema ana imani *ifikapo 2025 upatikanaji wa maji Dar es salaam utakuwa 100%.*


Pamoja na hayo *RC Makalla* amewapongeza DAWASA kwa *Mapinduzi makubwa Katika sekata ya Maji* na kueleza kuwa hivi karibuni *Serikali ya Mkoa itasaini Mradi mkubwa wa kuboresha Miundombinu ya Maji Taka Dar es salaam.*

0/Post a Comment/Comments