- Ni baada ya *kuchoshwa na Vifo vitokanavyo na ajali zitokanazo na Madereva kutoheshimu alama za Barabarani.*
- Achukizwa na *kutowajibika kwa Watendaji wa TANROAD*.
- Alitaka *Jeshi la Polisi na TANROAD kudhibiti ajali hizo.*
- *Wananchi wamshukuru kwa kusikiliza kilio Chao.*
- Madereva watakiwa *kuzingatia Sheria za Barabarani.*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewaelekeza *TANROAD* kwa kushirikiana na *Jeshi la Polisi kitengo Cha usalama Barabarani* kudhibiti tatizo la ajali *Barabara ya Morogoro eneo la Kiluvya kwa Komba* Kudhibiti tatizo la ajali eneo hilo kufuatia eneo hilo *kushamiri kwa ajali.*
Mapema leo asubuhi *RC Makalla* amefika eneo hilo na *kupokelewa na kundi la Wananchi* waliokuwa wamejiandaa *kulala Katika ya Barabara* kuzuia shughuli za usafiri Kama sehemu ya kufikisha *ujumbe kwa Serikali.*
Akizungumza na Wananchi hao *RC Makalla* ameonyesha *kuchukizwa na TANROAD* kupuuza Malalamiko ya Wananchi na maelekezo ya Serikali ambapo *August 31* wakati wa *zoezi la kusikiliza kero za Wananchi* Jimbo la Kibamba hoja hiyo iliibuka na *TANROAD* kuagizwa kushughulikia kero hiyo lakini *mpaka Leo hakuna utekelezaji.*
Kutokana na hilo *RC Makalla* amelazimika *kumpigia simu Meneja wa TANROAD* na kumtaka kufika *eneo la tukio* Kuangalia *Mpango sahihi wa kudhibiti ajali* kwenye eneo hilo.
Aidha *RC Makalla* ametoa wito kwa *Jeshi la Polisi* kutoa adhabu Kali kwa Madereva wasiozingatia *alama za Barabarani* huku akiwataka *Madereva kuzingatia Sheria za usalama Barabarani.*
Maelezo hayo yamepokelewa na *Jeshi la Polisi* ambalo limeahidi kusimamia na *kutekeleza Maelekezo yote yaliyotolewa na RC Makalla* huku likitoa wito kwa *Wananchi kuchukuwa tahadhari wawapo barararani.*
Kwa mujibu wa wakazi wa Kiluvya kwa Komba, *Wananchi wamekuwa wakipoteza maisha kwenye eneo la kivuko Cha watembea kwa miguu Kutokana na baadhi ya Madereva kutoheshimu alama za Barabarani.*
Post a Comment