Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amesema Maandalizi yote ya Tamasha kubwa la Burudani lililopewa jina la *DAR SUNSET CARNIVAL* Coco Beach yamekamilika ambapo *amewakaribisha Wananchi* kujitokeza kwa wingi kwenye *tukio Hilo la Aina yake.*
*RC Makalla* amesema Tamasha hilo litatawaliwa na *Burudani* za aina mbalimbali ikiwemo *Mziki mzuri kutoka kwa Wasanii akiwemo Barnaba, Sholo Mwamba, Gnako, Snura, Christina Bella, Kinata Mc, Mr Blue, Belle9 na wengineo* na kutakuwa na Michezo ya watoto na Michezo ya fukwe.
Akizungumza wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Wilaya, *RC Makalla* amesema dhamira ya Serikali ya Mkoa huo ni *kuboresha fukwe* ili ziwe sehemu Bora na rafiki kwa *utalii.*
Tayari *mandhari ya ufukwe* huo imeboreshwa na Wadau wa *kampuni zote za Vinywaji* zimekamilisha *Ujenzi wa Vibanda vya kisasa* ili kuhakikisha watu wote wanaofika kupumzika wanafurahia mazingira.
Post a Comment