Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewataka Wafanyabiashara Wanaofanya biashara *maeneo yaliyokatazwa* hususani Kariakoo kufika *Soko la Machinga complex* kwaajili ya kupatiwa nafasi Kutokana na Soko hilo kusaliwa na *nafasi 2,400 za Wafanyabiashara.*
*RC Makalla* amesema hayo alipotembelea Soko hilo na kueleza kuwa mpaka Sasa Zaidi ya *Wafanyabiashara 2,200* wamepatiwa maeneo ya kufanyia biashara na wanafurahia *biashara zinakwenda vizuri sokoni apo.*
Aidha *RC Makalla* amesema Serikali imedhamiria *kutatua changamoto zote za kibiashara kwenye maeneo walipopelekwa Wafanyabiashara* ikiwa ni pamoja na kuelekeza *LATRA* kufikisha huduma ya *Usafiri wa Daladala* kwenye maeneo hayo ikiwemo Soko la Machinga ili *kuchochea Biashara*.
Hata hivyo *RC Makalla* amesema ifikapo siku ya kesho ndio *mwisho wa watu kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa* Kutokana na muda wa *siku 12* alizoongeza kufikia *kikomo.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* amesema *zoezi la kuwapanga vizuri Machinga kwa Mkoa huo linakwenda vizuri* na kwa utulivu wa Hali ya juu Kutokana na *elimu iliyotolewa na Serikali na Viongozi wa Machinga.*
Post a Comment