Katibu Mkuu Chama
Cha SAU Majalio Kyara.
TAARIFA KWA UMMA
YAH; UZINDUZI WA KAMPENI YA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19
Chama cha sauti ya umma(SAU) tuna mpongeza Mhe.Rais SAMIA SULUHU HASSAN, Waziri Mkuu na Kamati nzima iliyoshiriki katika kufanikisha upatikanaji wa mkopo huu wa Tsh 1.3trillion kutoka IMF na kutengeneza matumizi sahihi, ya kiubunifu na bora zaidi kwa pesa hizi.
Pesa hizi pamoja na kwenda kusaidi kupunguza/kuondoa maambukizi ya uviko-19, pia zitaleta maendeleo kwa nchi na jamii yetu kwa kuleta AJIRA nyingi, elimu bora,Maji,huduma bora za afya n.k
Aidha tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuruhusu matumizi ya manunuzi ya SINGLE SOURCE kwa fedha hizi.Hii itasaidia miradi iliyokusudiwa kukamilika ndani ya muda unaotakiwa
Niwaombe Viongozi na Watanzania wote tutoe ushirikiano mzuri katika kampeni hii na kuweka maslahi ya Taifa kwanza na kwa uaminifu
Imetolewa na:
Majalio Kyara
Katibu Mkuu Chama Cha
SAU
Post a Comment