SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA BORA YA CHUO CHA BAHARI DMI.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara wakati akitembelea maeneo mbalimbali katika Chuo cha Bahari Cha Dar es salaam (DMI) picha na Mussa Khalid

.........................................................

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM 

Serikali imesema itaendelea kuimarisha miundombuni bora na kutenga bajeti ya kutosha ya kukisaidia Chuo cha Bahari Cha Dar es salaam (DMI) ili kiweze kutoa wanafunzi waliobora wa fani ya ubaharia. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara wakati akifanya ziara katika Chuo hicho na kusema licha ya kuwa miundombuni yake ni ya zamani serikali itaendelea kuonyesha ushirikiano kwa chuo hicho ili kiweze kuwa katika hali ya ubora wa Kimataifa.

Aidha Naibu Waziri Waitara amesema kuwa lengo la serikali ni kuendelea kukiimarisha Chuo hicho kuwa na mazingira wezeshi kwani kinasaidia kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri pamoja na kuonyesha uzalendo kwa Taifa.

‘Kwa kuwa Dunia imeendelea sana kiteknolojia hivyo na hapa kunatakiwa kuboreshwa kuwa kwa kisasa ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufundishia visiwe vya zamani’amesema Naibu Waziri Waitara

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Bahari DMI Dkt Erick Massami amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa nchini kutokana na kuwa takriban asilimia 90 ya vijana wengi wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali wamepata mafunzo katika Chuo hicho.

Dkt Erick amesema wanaendelea kushirikiana na Mashirika Binafsi ili kuhakikisha elimu wanayoitoa ni ya kiwango ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema ajenda ya Uchumi wa Blue.

0/Post a Comment/Comments