
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba
(kulia) akiweka saini katika Mkataba wa
Msaada kati ya Serikali za Tanzania na
Sweden na (kushoto) ni Balozi wa
Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg
................................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepatiwa msaada kiasi cha Krona za Sweden milioni 750, sawa na shilingi bilioni 195.92 kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR II).
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika hafla ya Kusainiwa Kwa Mkataba wa Msaada kati ya Serikali za Tanzania na Sweden ambapo umeelezwa kuwa utasaidia kuleta mafaniko makubwa kwa kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa elimu na kuwezesha idadi kubwa ya watu kuchangia ukuaji wa uchumi.
Akizungumza katika Hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba ameeleza mafanikio ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo Awamu ya kwanza kutoka mwaka 2014/15 hadi 2020/21 kuwa ni pamoja na Ujenzi wa madarasa 10,409, vyoo 20,507, mabweni 646, nyumba za walimu 91, majengo ya Utawala 37, maktaba 49, na uchimbaji wa visima vya maji katika shule 16.
‘Haya ni mafaniko makubwa kwa kuwa yatasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa elimu na kuwezesha idadi kubwa ya watu kuchangia ukuaji wa uchumi’amesema Tutuba
Aidha amesema mpango huo utatekelezwa kwa miaka mitano kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu msingi na kwamba serikali itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kwa ufanisi.
Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg amesema kuwa wataendelea kuonyesha ushirikiriano kwa serikali ya katika kuhakikisha wanatoa elimu iliyobora .
Balozi huyo amesema serikali ya Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania kuyafikia malengo yake Hasa katika sekta ya elimu.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,amesema mkataba huo ambao wameusaini utasaidia kuendeleza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa usawa wakike na wa kiume watanufaika
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Mipango Emmanuel
Tutuba amesema Serikali itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mpango huu unatekelezwa
kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Post a Comment