SERIKALI YATOA BARAKA KUFANYIKA MKUTANO WA IMANI, UPENDO NA MIUJIZA DAR

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikutano sita mikubwa ya injili itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na James Salvatory

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Amosi Makalla,amesema Serikali ya awamu ya sita chini Rais wa Jamhuri wa Muungano,Samia Suluhu Hassani,itaendelea kuwaheshimu viongozi wa dini kwakuwa wanamchango mkubwa kwa Taifa.

 

Makalla amesayesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ,kuzungumzia Mkutano mkubwa wa  wainjilisti uliopewa jina la Imani,upendo,Miujiza ambao unatarajiwa kufanyika maeneo tofauti kuanzia octoba 6 mpaka octoba 10 mwaka huu.

 

Amesema Rais Samia anatambua mchango wa viongozi wa dini kwa hatua yao ya kuliombea taifa liwe na amani pamoja na kuchangia katika shughuli za Maendeleo.

 

Aidha,Makalla,amesema serikali ya Rais Samia imetoa ruhusa ya kufanyika ya kwa mikutano hiyo kwa kutambua mchango wao ambapo amedai fursa kama hiyo haipatikani sehemu nyingine.


 

Hata hivyo,Makalla,Amewata watanzania wanaojitokeza kwenye mikutano hiyo  kuzingatia taratibu za wizara ya afya za kuchukua tahadhari ya uviko 19.

 

Kwa Upande wake  Askofu,Silvester Gamanywa,akizungumza kwa niaba ya viongozi dini,amesema mikutano hiyo pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la kuliombea taifa pamoja na Rais Samia

 

Naye Mwinjilisti Daniel Kolenda  amesema  kupitia kauli yao ya imani,upendo na Miujiza watafanya hafla sita za injili kuanzia leo Oktoba 06 kuanzia saa tisa jioni.

 

Mikutano inayoanza leo inatarajia kufanyika Maeneo sita tofauti Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya uchukuaji wa tahadhari ya uviko 19

 

0/Post a Comment/Comments