TAASISI YA MWALIMU NYERERE KUFANYA UZINDUZI 06.11.2021JIJINI DAR ES SALAAM

Safu ya viongozi wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwl.JK Nyerere



 Mwenyekiti wa taasisi ya mwalimu Nyerere mzee Paul Petro Kimiti.


*****************************************


NA RICHARD MRUSHA


Uzinduzi wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere unatarajiwa  kufanyika tarehe 06.11.2021 katika ukumbi wa Mwl.Julius Nyerere International convetion Centre jijini(JINCC) Dar es salaam.


Hayo yamejiri  katika Mkutano Mkuu wa wanachama wa Taasisi hiyo mbele ya Mwenyekiti wake Mh. Paul kimiti wakati akizungumza na wanachama waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jumapili tarehe 24.10.2021 katika ukumbi wa Msasani Beach kawe  jijini Dar es salaam.


Kupitia kwa katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Mh.Simon Rubugu baada ya kushauriana   na Mwenyekiti na   wajumbe bodi kwa pamoja  amesema uzinduzi  wa tukio hilo muhimu la kitaifa na la kihistoria litafanyika kama ilivyopangwa na halitoahirishwa.


Aidha katika hatua nyingine ndani ya  Mkutano huo wa wanachama wa Taasisi hiyo kulifanyika harambee ya kusaidia kuwezesha  Maandalizi ya uzinduzi,  kwa wanachama mbalimbali kujitokeza na  kujitolea kuchangia kwa hiari  ili kufanikisha tukio hilo muhimu la uzinduzi.



Katika harambee hiyo jumla ya shilingi Laki tano na themanini na tano(Laki)  585 000Tshs.) Zilipatikana zikiwa ni fedha taslimu ukumbini hapo huku shilingi milioni tano laki tatu na hamsini na tano elfu  zikiwa ni ahadi(Mil.5.355 Tshs) kutoka kwa baadhi ya wanachama hao waliohudhuria katika mkutano huo.


Pia katika mkutano huo wanachama mbalimbali waliokamilisha fedha za usajili wa uanachama walipata usajili wa kutambulika rasmi kwa mujibu wa katiba  ndani ya taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kupatiwa kadi na  Tshirt kwa waliokamilisha fedha za malipo kwa huduma hizo kabla ya tukio lenyewe la uzinduzi.



Katika mkutano huo uliohudhuriwa na  wanachama kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini, Pia ulihudhuriwa na viongozi kadhaa  waliohudumu  serikalini kitaifa  akiwemo  Spika Mstaafu wa Zanzibar Mh.Pandu Ameir Kificho, Mh Prof.Anna Tibaijuka Mh.Zakhia Meghji,   Mh.Dkt.Maua Daftari, Mh.Bi Imelda Mutafungwa(Mstaafu UN)  pamoja na katibu Mkuu Mstaafu wa ccm Taifa Mh.Wilson Mukama pamoja na Balozi Mstaafu Mh.Francis Mndolwa.



 viongozi hao wastaafu kwa nyakati tofauti hawakusita kutoa pongezi zao za dhati kwa Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mh.Paul Petro Kimiti  na sekretarieti yake   kwa  namna ilivyojipanga katika kuhakikisha Taasisi hiyo inayaenzi yale yote yaliyokuwa yakifanywa na hayati Baba wa Taifa Mwl.JK Nyerere enzi za uhai wake.

0/Post a Comment/Comments