
Waziri wa Maliasili na
Utalii nchini Dkt Damas Ndumbaro(kulia) wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam
.................................................................
NA MUSSA KHALID,
Serikali imesema inaendelea kuimarisha na kukuza
sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za kutangaza utalii huo
nchini ili kuweza kuwavutia wageni kutoka maeneo mbalimbali Duniani.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Dkt Damas Ndumbaro wakati akizungumza na
waandishi wa habari akitoa aarifa ya Tanzania kutajwa kuwa mwenyeji wa Onyesho
la Kwanza la Utalii katika nchi za Afrika Mashariki linalotarajiwa kufanyika
tar 9 - 16 mwezi huu jijini Arusha.
Waziri Dkt Ndubaro amesema katika kuunga mkono
Royal Tour ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan
ameianzisha Wizara hiyo imefuta tozo za utalii kwa muda wa wiki moja kwa wale
waliojisajili ili tamasha hilo lipewe heshima inayostahili.
Aidha Waziri Dkt Ndumbaro amesema kutokana na nchi
ya Tanzania kuandaa onyesho hilo ni heshima kwa nchi kwani litakuwa na manufaa
makubwa kwani itasaidia kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini.
Hata hivyo amewataka watanzania wakiwemo Waongoza
Utalii pamoja na Vyama vyote wa Utalii nchini kuweza kutumia fursa hiyo
kushiriki katika tukio hilo muhimu ambalo kwa mara ya kwanza linafanyika nchini
Tanzania.

Post a Comment