TIMU YA UHAMIAJI FC YATAKA KUFANYA MAPINDUZI LIGI KUU YA ZANZIBAR MSIMU WA MWAKA 2021/2022.


Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makakala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jezi za Uhamiaji FC itakayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao.

Msemaji wa Timu ya Uhamiaji FC Mwinyi Hamad akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jezi za Uhamiaji FC itakayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao.

Muwakilishi kutoka AZAM ambao ndio wadhamini wa Timu hiyo Egbet Mpinzile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jezi za Uhamiaji FC itakayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao.



 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makakala ,Kamishna wa Uhaiaji Uraia na Paspoti Gerald Kihinga Msemaji wa Timu ya Uhamiaji FC Mwinyi Hamad, Muwakilishi kutoka AZAM Egbet Mpinzile wakiwa waishika jezi maalum itakayotumiwa na Timu ya Uhamiaji FC katika michezo yake ya ugenini  na nyumbani  (picha zote na Mussa Khalid).

................................

NA MUSSA KHALID. 

Wakati michuano ya ligi kuu ya Zanzibar ikitarajiwa kuanza kurindima kuanzia Oktoba 30 mwaka huu Timu ya Uhamiaji FC itakayoshiriki ligi hiyo imezindua Jezi maalum watakazo zitumia katika michezo yao kwenye msimu wa mwaka 2021/2022. 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt Anna Peter Makakala amezindua jezi hizo leo katika eneo la Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyoko Kurasini  jijini Dar es salaam na kusema timu hiyo imeanza safari ya kupanda ligi kuu ya Zanzibar kwa muda mrefu hivyo matarajio yao ni kuhakikisha wanachukua ubingwa wa ligi hiyo. 

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt Makakala ameyapongeza makampuni ya Azam kutokana na kutoa udhamini wa Timu hiyo kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali yakiwemo mavazi (Jezi),vifaa pamoja na fedha taslim. 

Awali akizungumza Msemaji wa Timu ya Uhamiaji FC Mwinyi Hamad amesema timu hiyo inakwenda kufanya maajabu katika ligi kuu ya Zanzibar na hivyo kuiheshimisha kwani mdhamiwi wao amewasaidia mahitaji muhimu hivyo watachera Pira visa na pira Paspoti.

Kwa upande wake Kepteni wa Timu ya Uhamiaji FC Issa Hamis Ngao wamemuhakikishia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kuwa watakwenda kupambana ili waweze kupata ushindi wa ligiu kuu ya Zanzibar.

Muwakilishi kutoka AZAM ambao ndio wadhamini wa Timu hiyo Egbet Mpinzile amesema wameanza kwa kutoa fedha taslim Mill 50 kuidhamini timu hiyo hivyo watahakikisha wanaendelea kuwaonyesha ushirikiano katika michezo yao.

0/Post a Comment/Comments