Na Mwandishi wetu Dar
Imeelezwa kuwa Uvaaji wa miwani pasipo kushauriwa na Mtaalamu na kubandika kope wako hatari kupata matatizo ya macho ikiwemo upofu.
Hayo yamesemwa Juzi na Mtaalamu wa macho kutoka Taasisi ya Vision Care Eyes Clinic Careen Mashayo wakati wa zoezi la upimaji macho katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani ya Magufuli jijini Dar es Salaam Ikiwa ni mwendelezo wa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Afya ya macho.
Amesema ni muhimu watu kukutana na wataalamu wa afya na kupima macho kabla ya kuvaa miwani hata za urembo.
Amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa asilimia moja ya watanzania ni vipofu huku wengine asilimia 55 wakiwa na tatizo la uoni hafifu.
Kwa upande wake Mratibu wa afya ya macho Mkoa wa Dar es Salaam ,Dk Patrick Kabangut'se amebainisha kuwa asilimia mbili ya watu wanaofika kwenye huduma wanagunduliwa kuwa na matatizo ya macho kwa mkoa huo.
Naye Rais wa Wataalamu wa Macho Tanzania,Eden Mashayo amesema wanatarajia kupima watu 300 katika huduma hiyo ya siku moja.
Amesema mwitikio wa watu kujitokeza kupima macha katika stendi hiyo umekuwa mzuri.
Post a Comment