Baadhi ya wahitimu wa taaluma mbalimbali katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM)
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Takriban wanafunzi 4,298 waliohitimu na kutunikiwa Shahada,Stashahada na Astashada mbalimbali katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) wametakiwa kutumia elimu waliyoipata kama ushawishi kwa watu wote ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika Jamii na Taifa.
Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam katika mahafali ya 51 ya Chuo hicho ambapo Mgeni Rasmi, Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM),Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku vyeti wahitimu hao kutoka katika Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia,Ndaki ya Insia,Ndaki ya Teknolojia za habari na Mawasiliano,shule kuu ya Biashara,madini,na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
Akizungumza katika hafla hiyo,Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Anangisye amewataka wanafunzi hao kutosubiri kuajiriwa bali wakawe wepesi kuangalia ujuzi wao katika ufanyaji wa kazi hata kwa kujitolea.
‘Kwa wale munaorudi kwenye vituo vyenu vya kazi ni matarajio yeutu kuwa mtaongeza tija katika majukumu yenu ya kila siku hivyo nawasihi sana pamoja na mambo mengine muhimu musisahau kuwa wazalendo’amesema Profesa Anangisye
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho,Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewasihi wanafunzi hao wawe werevu katika kukabiliana na changamoto za kimaisha watakazokumbana nazo sambamba na kufanya kazi kwa bidii kwa kutafuta fursa za kujiendeleza kimaisha.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa taaluma mbalimbali katika chuo hicho wamesema watakwenda kuhakikisha wanafanyia kazi yale waliyojifunza kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Hata hivyo imeelezwa kuwa kutokana na changamoto zinazotokana na Ugonjwa wa UVIKO 19 zimesabaisha kuathiri shughuli mbalimbali zikiwemo makongamano,utafiti lakini pia wanafunzi wa kigeni hawakuweza kurudi chuoni.
Post a Comment