WANANCHI WAASWA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MBIO MBALIMBALI.

Na Mwandishi wetu 

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Mheshimiwa Hassan Masala amewaomba Wananchi kujitokeza kushiriki mbio mbalimbali fupi na Ndefu Ili kujenga mwili kimazoezi na kuimarisha Afya zao.


DC Masala ameyasema hayo leo kwenye kilele cha mbio za Rock City Marathon ambazo zimefanyika Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza na kushirikisha wakimbiaji zaidi ya elfu Moja.


Mheshimiwa Masala amesema Serikali inaendeleaa kuweka Mazingira rafiki katika Michezo yote hasa riadha ili kuandaa vijana wengi wenye Vipaji Ili kushiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi.


"Michezo ni fursa na fursa lazima tuitumie kuanda vijana wanamichezo wanatakaoliwakilisha Taifa kwenye mashindano ya kitaifa na Kimataifa" alisema DC Masala.


"Kama Wilaya ya Ilemela tumeshaanzisha Ilemela Jogging Club na huwa tuna mbio za Kila mwezi na washiriki wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku kukimbia Ili kuimarisha Afya zao na kuondoa magonjwa nyemelezi" Alisema DC Masala.


Mashindano ya Rock City Marathon yamekamilika leo katika huku Mtanzania Alphonse Simbu alishinda kilomita 21 na Mwanadada Mkenya Cheruta Ester akishinda kilomita 21 huku DC Masala akishiriki kilomita 10.






0/Post a Comment/Comments