Rai hiyo imetolewa leo na katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuhuisha Tabia za Kiislamu Tanzania (JAI), Saad Ahmed Salm wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwao Ilala jijini Dar es salaam ambapo amesema wamekuwa wakichangia Damu kwa kila baada ya miezi Minne hivyo watu waone umuhimu wa kujitoa kuwachangia wahitaji wa Damu salama.
Aidha amesema kuwa mahitaji ya Damu hapa nchini yamekuwa makubwa na muhimu ikiwemo kwa Majeruhi, watoto walio chini ya miaka Mitano,Wajawazito,wagonjwa wa Saratani na wenye magonjwa ya kuhitaji Damu.
Katika hatua nyingine amesema kuwa JAI imeweza kupewa tuzo ya heshima kutoka hospitali ya mkoa wa Amana kutoka kwa waziri wa Afya Dkt Doroth Gwajima kwa jitihada zao za kuchangia Damu.
Hata hivyo Katibu huyo amevishukuru vyombo vya habari hapa Nchini na taasisi mbalimbali kwa kuwaunga mkono katika jitihada zao za kuihudumia Jamii ikiwemo Radio Times Fm, huku akiwataka watanzaia kujikinga na kujitokeza kupatiwa chanjo ya Uviko 19.
JAI ni taasisi ya kijamii inayojihusisha na shughuli za utoaji wa huduma zote stahiki kwa wagonjwa waliopo Hospitalini na majumbani bila kubagua jinsia,rangi kabila au Dini,

Post a Comment