BODI ya Filamu imeipongeza tasnia ya filamu nchini kwa kufanikiwa kuchaguliwa kwa Filamu ya Nyara na Mulasi kuwania tuzo ya Like international Pan African Film Festival zinazotarajia kufanyika nchini Nairobi Kenya Novemba 3 hadi 6, 202.
Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kukabidhi bendera wasanii hao, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu, Kiagho Kilonzo, amewapongeza na kuwataka watanzania kuwaombea waweze kurudi na tunzo.
"Filamu ya Nyara ambayo imefanya vizuri na imefanikiwa kushinda tuzo ya Zanzibar Internationa Filam Festival ZIFF kama filamu bora na sasa inaenda kushindana nchini Kenya kama filamu bora na mwigizaji bora wa kiume anawania Cojack Chilo.
Pia filamu ya Mulasi imeingia kama filamu bora na Mwigizaji bora wa kike anawania tuzo ni Rejina Kihwele, 'Gynah' anawania na wasanii kutoka nchini Afrika kusini, Cameroon na Uganda.
Aidha ameongeza kuwa serikali imeanza kutoa udhamini kwa waandaaji wa filamu wanatakiwa kuandaa zenye maadili na kuangalia mira na desturi ya mwafrika nasio kuiga ughaibuni.
Kwa upande wake msanii Regina Kihwele, ambaye ameteuliwa kuingia kwenye kinyanganyilo cha msanii bora wa kike amesema kuwa niwakati wa Tanzania kuonyesha uwezo wetu kimataifa.
Naye Cojack Chilo ameingia kwenye kinyanganyilo cha filamu bora ya Nyara na kugombea msanii bora wa kiume kupitia filamu ya Nyara ambayo imefanya vizuri zaidi.
Post a Comment