Wananchi wa Tanzania wameombwa kuwa na tabia ya kumngoja Mungu katika vipindi mbalimbali ambavyo wanakutana navyo kila Wakati.
Haya yamesemwa na Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Tanzania Sarah Magesa Kupitia wimbo wake mpya uitwao Bado Nakungoja.
Sarah amesema kuna wakati Watanzania tunapitia vipindi vigumu na vingine vyepesi, kikubwa ni kuendelea kumngoja Mungu kwa Saburi.
"Ukiangalia kama nchi tunapitia vipindi tofauti vingine vinavunja Moyo na vingine vinaumiza kama wakati huu wa Ugonjwa wa Corona, tusiache kumtegemea na kumngoja Mungu atushindie" alisema Sarah Magesa.
Wimbo wake Sarah Magesa uiitwao Bado Nakungoja umerekodiwa hivi karibu na Ukiwa na ujumbe wa kuwasihi watu wote kuwa na tabia ya kumngoja Mungu katika mambo yote.
Wimbo huo unapatikana Kupitia Mtandao wake wa YouTube na Mitandao mingine ambayo Nyimbo mbalimbali zinawekwa hapo.
https://youtu.be/UopgMotLQNA

Post a Comment