Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro
...............................
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya afisa mtendaji wa Serikali ya mtaa wa Mbezi Msumi aliyefahamika kwa jina la Kelvin Costa Mowo miaka 38, Mkazi wa Bunju.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro Akizungumza mapema leo amesema kuwa Tukio hilo limetokea jana Oktoba 11,2021saa11:54 asubuhi huko eneo la Msumi Mbezi wilaya ya Ubungo katika ofisi za Serikali ya mtaa huo,
Kamanda Muliro amesema kuwa marehemu akiwa ofisini kwake akisikiliza mgogoro wa ardhi Ghafla watu wapatao wanne waliingia ofisini na mmoja wao akatoa panga na kumshambulia mtendaji huyo kitendo kilichopelekea kupata majeraha makubwa na baadae kupoteza maisha wakati akikimbizwa hospitalini.
Amesema watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo wakihojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani.
Post a Comment