Mkurugenzi Mtendaji wa –Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC) Dkt Maduhu Kazi
.....................................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Zaidi ya makampuni matano kutoka Jamhuri ya Czech yanakusudia kuwekeza Nchini katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo hasa katika zao la pambana viwanda vya nguo.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam baada ya mazungumzo kati ya kituo cha uwekezaji Nchini –TIC pamoja na jamhuri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa –TIC, Dkt Maduhu Kazi amesema tayari Serikali imewahakikishia wawekezaji hao mazingira mazuri ya uwekezaji.
Mkurugenzi huyo amesema ujumbe huo wa wafanyabishara kutoka Jamhuri ya Czech baada ya mazungumzo wameonesha nia ya kuwekeza katika Viwanda vya nguo, uunganishaji wa ndege ili kuchochea maendeleo nchini.
‘Sekta nyingine ambayo wawekezaji hao wamevutiwa nayo ni pamoja na uwekezaji katika ufundi wa ndege pamoja na utengenezaji wa ndege ndogo zinaweza kuhusika katika maswala ya kiuchumi’amesema Dkt Maduhu
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Posi amewataka wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa ya kupata wabia wa kibiashara ili kuchochea ukuaji wa sekta ya uwekezaji na kuachana na dhana ya kila kampuni kubwa kutoka nje lazima mbia wake awe serikali.
Naye Naibu waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech Miloslav Stasek amesema ziara hiyo itafungua milango kwa wafanyabishara kutoka nchini humo kuja kuwekeza nchini kutokana na vivutio vya uwekezaji walivyoviona.
Ujumbe kutoka Jumhuri ya Czech umeambatana watu kutoka Wizara ya mambo ya Nje,Wizara ya Fedha na wafanyabisha kwa lengo la kufanya mazungumzo na kuona fursa za uwekezaji nchini.
Ujio wa wawekezaji hao umeambatana na waziri wa mambo ya nje ya jamhuri wa cheki Injinia Miloslav Stazek ambapo wamebetelembea taasisi na wizara mbalimbali ikiwa ni pamoja na wizara ya viwanda na biashara.
Post a Comment