Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MSANII wakike kutoka Lebo ya wasafi (WCB) inayofanya vizuri nje na ndani ya nchi, Zuhura Othman maarufu kama Zuchu awatolea makavu baadhi Makampuni pamoja na watu kwa kitendo cha kuwadharau watoto wakike.
Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wakijamii wa "Instagram" wa zuchu ameandika .
"Nasikitishwa sana na baadhi ya watu au Kampuni ambao tunafanya nao Kazi,ifike muda Msanii aheshimiwe katika status na platform yake inayotumika kutangazia kitu Fulani.
Hata hivyo Zuchu hakushia hapo aliendelea kwa kusema kuwa .
"Hii sio favor Wala sio Msaada, tunafanya kazi kwa Makubaliano basi ifike hatua mjifunze kuheshimu wasanii."
Pia akafafanua kuwa "Kinachomkera zaidi ni kwamba wanajua unafanya kazi kubwa kushikilia bango kwa kiasi kikubwa kuchangia ushawishi kwenye matumizi ya kampuni zao.
Nakumalizia kuwa " watu wengi au Makampuni mnadharau sana wanawake kwenye upande wa malipo.
Post a Comment