ABDULL KAMBAYA NA WENGINE SITA WATIMULIWA UANACHAMA CUF.

Mkurugenzi  wa habari, uenezi  na mahusiano na  umma  Injinia  Mohamed  Ngulangwa
.........................

SALIM BITCHUKA 

Chama   cha  Wananchi ( CUF)  Kupitia   Baraza  kuu  la  Uongozi  la Taifa  la  chama    hicho  limewavua  uanachama  waliokuwa  wanachama  wao  saba  kwa  kosa  la  kula  njama  ya  kukihujumu  chama  kifutiwe  usajili .

Akiwasilisha   taarifa  hiyo  leo jijini  Dar es  Salaam  Mkurugenzi  wa habari, uenezi  na mahusiano na  umma  Injinia  Mohamed  Ngulangwa   amesema  mbali na  kusimamishwa  kwa  wanachama  hao   Baraza  kuu  taifa  CUF  Pia  limewasimamisha  uachama  wanachama  watatu  na  wanne  kupewa  karipio kali  la Maandishi.

Injinia  Ngulangwa  amesema  pamoja  na  ukweli  kwamba   kila  mmoja  alikuwa na  mashitaka  yake  asilimia  50  ya  viongozi   hao  walishirkiana  kula  njama ya  kukihu jumu  chama.

Aidha  Mohammed  Ngulangwa  amewataja  waliovuliwa  uanachama  ni  pamoja  na aliyekuwa  mjumbe  wa Baraza  kuu la  Uongozi  kanda  ya  Pwani  Abdalla  Juma Kambaya, Mkurugenzi   wa Mipango  na uchaguzi  Mohamed  Vuai  Makame, Alli  Makame  Issa na Chande  Jidawi.

Wengine  waliovuliwa  uanachama  ni   pamoja  na  Hamida  Abdallah  Huweishil, Dhifaa  Mohammed  Bakari   na  Mtumwa  Ambar Abdallah.

Maazimi  hayo   yamepitishwa  na  Baraza  kuu  la  Uongozi  la  Taifa  la chama  cha  Wananchi  CUF  walipoketi  Novemba  5  na  6 mwaka  huu 2021 huku  likijadili masuala  mbali mbali pamoja  na  kumthibibitisha  Mbarouk Seif  Salim  kuwa  mjumbe wa  Baraza kuu,na pia  Baraza  limempitisha  kuwa  Naibu  Katibu  mkuu  Zanzibar   huku  Mwadini  Jecha  akiteuliwa  kuwa   Mkurugenzi  wa  Mipango  na Uchaguzi.

0/Post a Comment/Comments