Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Dkt.Julius Ningu
akielezea mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 86 katika Wilaya ya
Namtumbo ambapo aserikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kutekeleza
mradi huo
Mkuu wa shule ya sekondari Nasuli wilayani Namtumbo akizungumza
mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa utakavyopunguza uhaba wa vyumba
vya madarasa katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 1200 ikiwa na vyumba 22
na upungufu wa vyumba nane vya kusomea
picha ya pamoja Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo katikati Dkt.Julius
Ningu na kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari Nasuli wilayani Namtumbo
ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari
Nasuli wilayani Namtumbo ambapo ujenzi umefikia hatua ya kuweka linta.
..................................
SERIKALI
ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu Hassan imeipatia Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kiasi cha
shilingi bilioni 1.6 kujenga vyumba 86 vya madarasa.
Mkuu
wa Wilaya ya Namtumbo Dkt.Julius Ningu akizungumza katika mradi wa ujenzi wa
vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya sekondari Nasuli mjini Namtumbo,amesema
theluthi moja ya madarasa 86 imefikia hatua ya lenta na ujenzi unaendelea kwa
kasi.
“Hadi
kufikia Jumamosi ya wiki hii majengo yote ya vyumba vya madarasa 86 katika
Wilaya ya Namtumbo yatakuwa yameshafungwa lenta na kujiandaa kuezeka wiki
inayofuata’’,alisisitiza Dkt.Ningu.
Hata
hivyo amesema mifumo mizuri ya usimamizi wa madarasa hayo kwa kuwatumia
wenyeviti wa Kamati za Ujenzi wananchi wenyewe kutoka maeneo ya mradi, kumesababisha
utekelezaji wa mradi huo kufanyika ndani ya wakati.
Amesema
kutokana na maelekezo ya serikali kukamilisha mradi wa madarasa kwa wakati,
walijiwekea utaratibu wa kufanya ujenzi kwa awamu kuanzia ujenzi wa
msingi,boma,kufunga lenta na kuezeka na kwamba awamu za ujenzi zilikwekwa kwa muda maalum wa siku
nne hadi saba katika kila hatua ya ujenzi hali iliyosababisha mradi kwenda kwa
kasi kubwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Nasuli Mwalimu Dafrosa Chilumba
ameipongeza serikali kwa mradi wa vyumba vitatu vya madarasa ambao amesema
utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule yake.
Chilumba
amesema sekondari hiyo ina jumla ya wanafunzi 1211 wanaosoma katika madarasa 22
na kwamba shule hiyo ilikuwa na upungufu wa vyumba nane hivyo kuongezeka kwa vyumba vitatu vya
madarasa kumepunguza kero ya uhaba wa madarasa katika sekondari hiyo yenye
kidato cha kwanza hadi cha sita.
Hadija
Khamisi ni Mwanafunzi wa kidato cha Tano katika sekondari ya Nasuli,ameipongeza
serikali kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa ambavyo amesema vitapunguza
msongamano wa wanafunzi madarasani hivyo walimu na wanafunzi kushiriki vema
katika kufundisha na kujifunza.
MKOA wa Ruvuma umepokea shilingi bilioni 12.7 sawa na asilimia 2.4 ya shilingi bilioni 635.68 ambazo zimeidhinishwa na TAMISEMI kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya Afya,Elimu na Uwezeshaji wananchi kiuchumi
Post a Comment