CANAF 2021 UGANDA 1 TZ 0



Timu ya Uganda  imeshinda goli mmoja dhidi ya wenyeji Tanzania  leo  Novemba 29, 2021 kwenye mashindano yanayoendelea  ya Afrika  ya soka  kwa wenye ulemavu CANAF 2021 katika  Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Goli la ushindi la Uganda limefungwa dakika ya 20  kipindi cha kwanza na mshambuliaji Ssempija Julius baada ya kuwahadaa mabeki wa Timu ya Tembo ya Tanzania.

Katika mchezo wa kwanza Tanzania iliibamiza timu ya Morocco 2-1. Wakati Uganda katika mchezo wake na Sierra Leon walifungwa 3-0.

Mchezo huu umechezeshwa na  Luciano Antonio kutoka Angola, Mohamed Mwadini kutoka Zanzibar na David Mng'ong'o kutoka Tanzania.

Mechi nyingine zinazochezwa leo ni Sierra Leon na Morroco, Kenya na Zanzibar, Liberia na Gambia pia Nigeria na Misri

 

0/Post a Comment/Comments