COCACOLA BURIANI FESTIVAL KUFANYIKA NOVEMBA 20 VIWANJA VYA KIJITONYAMA




Na Mwandishi Wetu


WASANII wa Hip Hop, Bongo fleva na Taarabu kushiriki katika jukwaa moja la Birian Festival lililoandaliwa na Coca cola kwanza Novemba 20, mwaka huu katika viwanja vya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara na Masoko Coca cola kwanza, Wahida Mbaraka, amesema kuwa tamasha hili litakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.


"Kwa kuzingatia mapenzi ya wadau wa Birian na Coca cola, tamasha hili litasindikizwa na  Dulla Makabira, Weusi, Isha Mashauzi, Baba Levo, Stamina, Baddest, Twanga Pepeta na Dj D Ommy.


Aidha amesema tamasha litaanza asubuhi  hadi saa kumi na moja jioni bila kiingilio, kuanzia jioni kutakua kunaingia kwa kiingilio ili kupata burudani zaidi tutatoa na kinywaji.


Kwa upande wake msanii Stamina amesema kuwa watu wafike mapema wasikose burudani za kutosha, tutaanza na biriani na baadae kutakuwa na burudani za wasanii wote usipange kukosa.

0/Post a Comment/Comments