*************************************
Na Mwandishi wetu
KATIKA kuhakikisha inakuza kiwango Cha masoko nchini, Kampuni ya Masoko na Mawasiliano Kidigitali ya 'Dentsu Tanzania' imezindua wiki ya masoko yenye nia ya kuongeza ufanisi wa masoko kwa kutumia fursa zilizopo katika tasnia hiyo.
Akitangaza kufunguliwa kwa wiki hiyo inayotarajia kuanza rasmi Desemba Mosi hadi 3 Mwaka huu Mkurugenzi wa Dentsu Aegis Network Tanzania, Edward Shila, alisema wiki hiyo pamoja na mambo mengine itawasaidia wataalam wa fani ya masoko, mawasiliano na mahusiano kuongeza ujuzi.
Alisema kupitia wiki hiyo, wataalamu hao watapata fursa ya kutengeneza mpango kazi mzuri wa shughuli za masoko na mawasiliano na kuzitumia vyema katika utaratibu utakaosaidia utoaji wa takwimu sahihi katika masoko.
"Lengo nivkuwawezesha wataalamu wa fani ya Masoko, Mawasiliano na Mahusiano kuzibainisha na kuzitumia fursa zilizopo kwenye fani hiyo nchini, hatua tunayoamini kuwa itasaidia kuleta ufanisi katika tasnia nzima" alisema Shila
Alisema chini ya kauli mbiu ya wiki hiyo kwa mwaka huu inayosema” Takwimu kwenye uendeshwaji wa masoko” wanaamini kwa kutumia matumizi ya takwimu ni muhimu katika kutengeneza mazingira bora na ufanisi.
Aidha alisisitiza umuhimu wa kujenga haiba ya wekezaji kwenye Vyombo vya Habari, Ubunifu katika Mawasiliano na Digitali kwa ajili ya kupata matokeo bora zaidi ya kiutendaji.
Alisema pamoja na mambo mengine kutakuwa na mijadala mbalimbali itakayoshirikisha wadau wa fani hizo kujadili njia nzuri za kufanya kazi kwenye fani mbalimbali.
Post a Comment