NA MUSSA KHALID.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku tuzo Jumla ya wahitimu 1,521 kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE), Digrii za awali Katika fani mbalimbali na 44 shahada ya uzamili na Digrii za Umahiri na kutakiwa kutumia maarifa yao katika kukuza uchumi wa nchi kuwa na Maendeleo.
Hayo yamejiri katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Nne ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es salaam ambapo Rais Mstaafu Dkt Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ametumia fursa hiyo pia kukishauri Chuo hicho kuhakikisha wanazingatia uwiano sawa katika kutoa mafunzo kutokana idadi ya wanawake waliohitimu kuwa 690 huku wanaume wakiwa 875.
Akizungumza Katika Mahafali hayo Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es salaam Profesa Willium Anangisye amewataka wahitimu hao kutafuta fursa badalanya kusubiri fursa ziwafuate jambo ambalo sio rahisi Katika ulimwengu wa sasa.
"Wahitimu wanafahamu kuwa ingawa wao ndio waliokaa darasani, kwenda maktaba na kufanya utafiti, mafanikio yao yametokana na michango ya wadau wengi ikiwa ni pamoja na Serikali,familia, asasi na watu mbalimbali". Amesema Prof.Anangisye.
Kwa upande wake Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es salaam Profesa Stephen Maluka ameeleza mafanikio ya chuo hicho kuwa mwaka 2020/2021 Chuo kilitenga Shilingi Milioni 413.5 kwaajili ya mafunzo ya watumishi kati ya kiasi hicho, shilingi milioni 113.5 ni kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi
"Shughuli za kiutafiti zimeenda sambamba na kuongezeka kwa machapisho yanayotolewa na wanataaluma wa Chuo. Ili kuimarisha shughuli za kitafiti, jarida la Chuo liitwalo Journal Of Education, Humanities and sciences, ambalo lilipata hadhi ya Kimataifa mwaka 2017 limeendelea kuchapishwa’Rasi wa chuo
Kwa upande wake Mwakilishi wa wahitimu hao Bi.Amina Abdallah amesema watahakikisha wanazingatia wosia waliopewa kuhusu kwenda kujiajiri na kuacha kutegemea ajira za serikali pekee.
Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa licha ya mafanikio hayo Uviko-19 umeendelea kuathiri shughuli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani makongamano, tafiti na ubunifu, na shughuli nyingine zinazohusisha mikusanyiko ya watu zilifanyika kwa tahadhari kubwa au kwa njia za mitandao pale ilipobidi.
Post a Comment