Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba na GSM Group kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya Shilingi bilioni 2.1 kwa kipindi cha miaka miwili.
“Mkataba huu utaenda kunufaisha klabu za ligi kuu, mpira wa sasa ni fedha, hivyo GSM Group umeona kuendeleza soka letu kwa vitendo na siyo kwa maneno.
“Sisi wadhamini tuliona kuna uongozi imara wa TFF ndiyo maana tumeamua kuwekeza,” - Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Saidi Hersi.
.
.
#TimesFMDigital
Post a Comment