Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipita baadhi ya maeneo
katika eneo la Jangwani Dar es Salaam alipokwenda kusikiliza changamoto za
wakazi wa eneo hilo wanaotaka eneo la Jangwani kupatiwa Mwekezaji.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisisitiza jambo
wakati wa kikao na watendaji wa sekta ya ardhi, Mradi wa Uendelezaji jiji la
Dar es Salaam (DMDP) na wawakilishi wa Kampuni ya Jangwani Holding Ltd baada ya
kumaliza ziara ya kutembelea eneo la Jangwani Dar es Salaam alipokwenda
kusikiliza changamoto za wakazi wa eneo hilo wanaotaka eneo la Jangwani
kupatiwa Mwekezaji.
.............................
Na Munir
Shemweta, WANMM
Baadhi ya wakazi wa
Jangwani jijni Dar es Salaam wamemuaomba Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Mkazi Dkt Angeline Mabula kusaidia Mwekezaji kupatiwa eneo la
Jangwani ili waweze kulipwa fidia na kupisha eneo hilo.
Wakazi hao
waliwasilisha ombi hilo kwa Naibu Waziri Dkt Mabula alipotembelea eneo la
Jangwani kujionea mazingira ya eneo hilo kama ni salama kwa uwekezaji sambamba
na mipango ya mamlaka husika kuhusiana na eneo hilo.
Kampuni ya Jangwani
Holding Ltd imeomba kuwekeza sehemu katika eneo la Jangwani na kukubali
kuwalipa fidia wakazi wanaoishi hilo. Hata hivyo, uamuzi wa kutoa eneo hilo kwa
ajili ya uwekezaji unasubiri ushirikishwaji wa mamlaka husika ambazo ni Ofisi
ya Makamu wa Rais idara ya Mazingira, Halmashauri ya Jiji la Ilala pamoja na
Mradi wa Uendelezaji jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Wakizungumza katika
eneo hilo juzi wakazi hao walisema, wanachohitaji kwa sasa ni Mwekezaji
kupatiwa sehemu ya eneo la Bonde la Jangwani ili nao waweze kuwalipwa fidia na
kwenda kutafuta maeneo mengine ya kuishi.
Kwa mujibu wa Wakazi
hao, eneo hilo limekuwa na changamoto ya mafuriko kwa muda mrefu na juhudi za
awali za serikali kuwapatia maeneo wananchi Mabwepande wilaya ya Kinondoni
halikudhi wakazi wote kwa kuwa walipatiwa viwanja walikuwa 43 kati ya 1,200.
‘’ Imekuja Kampuni
inataka kutuhamisha hapa na itulipe fidia lakini mamlaka husika hazijaridhia
huku halmashauri ya jiji ikishindwa hata kuweka vibao kuonesha kuwa eneo hili
ni eneo hatarishi na maeneo yamewekwa vifusi na kuendelea na shughuli kama kawaida’’
alisema mwananchi mmoja.
Walisema kwa sasa wako
hoi bila ya kujua hatma yao na kuomba Mwekezaji kupewa eneo ili waondoke kwenda
kutafuta sehemu nyingine za kuishi kwa kuwa baadhi ya nyumba zao zimeharibika.
Salehe Selemani Cheyo
aliyejitambulisha kama Mjumbe wa Mtaa wa Msimbazi Bondeni alisema, kiu kubwa ya
wakazi wa eneo la Jangwani ni kuona mwekezaji anapatiwa eneo hilo ili waweze
kulipwa fidia na kudai kuwa kinachowashangaza ni kuelezwa eneo hilo ni atarishi
wakati limekuwa likipatiwa huduma mbalimbali kama vile maji na umeme na
wananchi wamekuwa wakilipia huduma hizo.
‘’Tunaambiwa eneo hili
ni hatariishi wakati watu tuna leseni za makazi na tumekuwa tukilipa kodi za
majengo na nyumba zipo mpaka Sambusa, kwanini hatarishi wakati pesa za wananchi
wanachukua? Alihoji Cheyo
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaomba wakazi wa eneo hilo
kuwa na subira wakati serikali ikilifanyia kazi suala hilo kwa kuwa kuna
mamlaka na mipango tofauti kuhusiana na eneo hilo ambapo serikali lazima zijiridhishe
kama uwekezaji hautakuwa na madhara sambamba mipango ya uendelezaji.
Kwa mujibu wa Dkt
Mabula, kabla ya uamuzi kufanyika lazima baadhi ya mamlaka zishirikishwe
ili maamuzi yatakayotolewa yawe na tija na mamlaka hizo ni pamoja na Ofisi ya
Makamu wa Rais idara ya Mazingira, Halmashauri ya Jiji la Ilala pamoja na kujua
Mradi wa Uendelezaji jiji la Dar es Salaam (DMDP) unasemaje kuhusiana na eneo
hilo.
‘’Mambo yakienda vizuri watawekeza lazima mvute subira na kilichonileta hapa ni kujiridhisha eneo ni salama, je liko katika mpango ganoi na wahusika wamejiridhisa? Maana hatuwezi kupitisha leo halafu kesho kunatokea maafa, naomba muwe na subira’’ alisema Naibu Waziri Dkt Mabula.
Post a Comment