Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa
Jeshi hilo,Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam.
...............................
NA
MUSSA KHALID.
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)
limewataka watanzania kuwaepuka na wasidanganyike na baadhi ya watu wanaofanya
utapeli na kuwalagha vijana kuwa wanawaandikisha kujiunga na Jeshi la kujenga
Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam
na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi hilo,Luteni Kanali
Gaudentius Gervas Ilonda wakati akitolea ufafanuzi kufuatia kuibuka kwa
mwenendo wa baadhi ya watu wakitumia fursa ya uandikishwaji wa vijana
kujinufaisha.
Luteni Kanali Ilonda amesema udanganyifu huo
unaofanyika umesababisha kuleta usumbufu kwa wananchi wenye vijana wao
waliokuwa kwenye Makambi ya Kujenga Taifa jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Aidha Luteni Kanali Ilonda amesisitiza kuwa
hakuna nafasi ya kuingia Jeshini kwa kutumia mgongo wa fedha hivyo ametoa rai
wa watu wanaohusika katika kuwalangai wananchi kuacha mara moja.
Amewata watanzania kuzifahamu taratibu mbalimbali za kujiunga na jeshi kuwa ni pamoja na kuwa raia wa Tanzani,Umri wa miaka 18-28,kuwa na afya njema ya mwili na akili lakini pia awe hajapatikana na hatia ya makosa yeyote ya jinai,awe na cheti cha kuzaliwa pamoja na cha taalum.
Post a Comment