KIMBEMBE,JOTI,KAZOA KUWANIA TUZO YA MCHEKESHAJI BORA




Profesa Martin Muhando akitangaza vipengele 30 vilivyoingia katika Mchakato wa kuwania Tuzo za Filamu zilizoandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu nchini.


Meneja vipindi wa kituo Cha Azam tv Fatma Mohammed akifafanua zaidi jinsi watazamaji wa Filamu walivyopatw nafasi ya kuzionq Filamu 122 zilizofanikiwa kupitia mchujo wa awali katika Kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu zilizoandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu nchini



Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


VIPENGELE vitavyochuana katika Kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu zilizoandaliwa na Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu vyatangazwa rasmi jijini Dar es salaam.


Akizungumza na waandishi wahabari pamoja na wadau wa tasnia ya Filamu ,Rais wa Shirikisho la Sanaa nchini (TAFF)Elia Mjata amesema Mchakato umezingatia haki hakuna janja janja.


"Nimekuwa Miongoni mwa watu ambapo wamefatilia mwanzo mchakato ulivoanza Hadi hatua ilipofikia ambayo ndio ya mwisho ili kupata nafasi ya kupigia kura majina au Filamu zilizofanikiwa kupitia kwenye mchujo ambao ulishirikisha Majaji ambao ni wataalamu katika tasnia yetu."


Hata hivyo Mjata ameongeza kuwa Tuzo hizo zinalenga kuboresha soko la Filamu na kuleta ushindani kutokana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua kuipa kipaumbele Sanaa.


 "Kwa mara ya kwanza Serikali imepitisha mkono wake na kuandaa Tuzo hizi kama sehemu ya kukubali kile tunachokifanya na kuwepo kwa kitu kama hiki inatia moyo kwa wasanii wetu kuendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi."


Hata hivyo Mjumbe wa Kamati ya Tuzo za filamu Martin Muhando ameeleza kwa namna gani anajivunia kuwa Mtanzania na anategemea Filamu zilizoingia kwenye Tuzo hizo zinaweza kutoboa ndani na nje ya nchi kutokana na ubora wake kuanzia utayarishaji wake,Mavazi,sauti na ubora wa picha jongefu.


Pia ametangaza takribani vipengele 30 vilivyofanikiwa kupata washiriki wa 5 kutoka katika tamthilia zilizoingia huku akitaja kipengele Cha 29 kukosa Washiriki kutokana na kutoendana na vigezo ilivyopaswa kufatwa katika Mchakato huo.


"Vipengele 30 vimeingia kwenye Kinyang'anyiro hicho Cha Tuzo za Filamu ikiwemo Msanii Bora wa vichekesho ambapo Said zubery (Kimbembe)Lucas Mhavile(joti) Hassani Kazoa (Kazoa)wanawania tuzo hiyo,Mtayarishaji bora wakike na wakiume,Filamu bora , Filamu bora ya vichekesho na vingine vingi huku katika kipengele Cha Filamu bora yenye utamaduni wetu nchini kukosa vigezo kutokana na kutokuwepo uhalisia hivyo ningependa wasanii kwa Mashindano yajayo waweze kulifanyia kazi Hilo."


Pia ameeleza kwa namna Majaji takribani 8 waliweza kutazama Filamu zipatazo 122 kwa usahihi ili na kuleta maoni yao kwa pamoja na kuwapa alama Filamu walizozitazama na amewatoa hofu kuhusu taaluma za Majaji hao kuwa ni bobezi na kuwataka Mashabiki wapige kura ipasavyo kwa vipengele hivyo.


Kwa upande wa Meneja programu wa kituo Cha Azam tv ameongeza kuwa Filamu hizo zilionyweshwa kwa kipindi husika na kuwaacha Mashabiki waweze kuona Filamu hizo zilizopata nafasi ya kuingia katika Mchakato.


"Filamu 122 zilionyweshwa zote kuanzia saa 8 mchana Hadi saa 12 muda ambao ni rafiki hivyo watazamaji walipata nafasi ya kuzitazama vizuri ili waweze kupata nafasi ya kuzipigia kura na kwa kuwatoa hofu tu Wadau wa Filamu na watazamaji kwa ujumla Tuzo hizi hakuna kubebana tunataka kura ya haki ili wewe uweze kuchagua kilichobora zaidi".


Pia Upigaji kura wa Tuzo hizo ni kupitia simu ya kiganjani kwa kutuma neno Tuzo kwa njia ya mtandao wa kijamii (Whatsapp) kwa kupitia namba ambazo zitatangazwa kupitia kurasa za Bodi ya Filamu na kwa mfatiliaji wa Tuzo hizo ataweza kufanikisha kupigia kura kipengele akipendacho.




.....Mwisho....

0/Post a Comment/Comments