MAMBO 10 ALIYOWEKEA MKAZO RC MAKALLA LEO KUHUSU KAMPENI ENDELEVU YA USAFI DSM


*"Kampeni ya Usafi sio ya Mkuu wa Mkoa pekee,* Ni jukumu la kila mmoja kuibeba kwa kufanya Usafi". *RC MAKALLA.*


"Tunaposema Usafi wa pamoja kila Jumamos ya mwisho mwezi *hatumaanishi Shughuli za kiuchumi zisimame,* Bali kila mmoja asafishe eneo lake na kuendelea na majukumu". *RC MAKALLA.*


"Uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Usafi DSM ni *Disemba 04* kata ya Kivukoni.  *RC MAKALLA*.


"Tunataka *kampuni za Usafi Dar es salaam za uhakika* na zenye vitendea kazi". *RC MAKALLA.*


*"Kampeni hii ya Usafi itafanikiwa kwa 100%* sababu tumetumia mfumo *Shirikishi, elimu na tumefanyia kazi changamoto* zilizokwamisha Kampeni Kama hizi zilizopita" *RC MAKALLA*.


"Tunapozungumzia Usafi DSM tunahusisha *Udhibiti, Usafishaji mazingira, Usafirishaji wa taka, Uteketezaji wa taka na uhamasishaji* kwa Wananchi kufanya Usafi" *RC MAKALLA*.


"Tunaboresha *Dampo la Pugu* na nimeelekeza *kila Halmashauri itenge fedha* ili kila moja iwe na Dampo lake" *RC MAKALLA*.


" *Maono yangu Ni Kuifanya Dar es salaam kuwa Jiji la Kisasa*, na ili kufikia huku nategemea ushirikiano wa Wananchi" *RC MAKALLA*.


"Nichukuwe Fursa hii kuwaomba *Wadau kutupatia Dustbin* za kuhifadhi taka" *RC MAKALLA.*


"Tutatumia zoezi la *kuwapanga Vizuri Machinga na Usafi Kama Kipimo Cha utendaji kazi kwa Watendaji* wa Mitaa". *RC MAKALLA*.


#Safisha Pendezesha Dar es salaam.

0/Post a Comment/Comments