Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Balozi wa
Tanzania nchini Jamhuri ya Visiwa vya Comoro kuratibu sekta binafsi pamoja na
Serikali ili kutumia fursa za kibiashara zilizopo nchini humo kuhakikisha Tanzania
inanufaika na mahitaji ya bidhaa mbalimbali katika nchi hiyo.
Mhe.
Rais Samia amesema hayo leo tarehe 07 Novemba, 2021 Ikulu Chamwino Mkoani
Dodoma katika hafla ya kumuapisha Mhe. Pereira Ame Silima kuwa Balozi wa
Tanzania katika Jamhuri ya Visiwa vya Comoro.
Pia,
Mhe. Rais Samia amesema mahitaji ya nchi ya Jamhuri ya Visiwa vya Comoro yanaitegemea
Tanzania kwa zaidi ya asilimia 80 hivyo kutoa fursa kubwa ya biashara kwa
Tanzania.
Aidha,
Mhe. Rais Samia amemtaka Balozi Pereira kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi
hizo mbili katika masuala ya kisiasa, sekta ya biashara na diplomasia kwa kuwa
Tanzania na Comoro zina historia ya uhusiano wa muda mrefu.
Hafla ya kumuapisha Balozi Pereira imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Katanga, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Vincent Mbogo pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Serikali.
Post a Comment