Afisa Masoko wa Huduma kwa wanachama kutoka
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Luhende Andrew Singu (picha na Mussa
Khalid)
................................
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Watanzania wametakiwa kupenda kujiunga na
mifuko ya Bima ya Afya ili kuwa salama kwa matibabu kutokana na na kuwa ugonjwa
hauipi hodi.
Akifanya mahojiano na mwandishi wa habari
hizi leo jijini Dar es salaam katika muendelezo wa maonyesho ya wiki ya kifedha
Afisa Masoko wa Huduma kwa wanachama kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF
Luhende Andrew Singu ambapo amesema ni vyema wananchi wakaacha utamadui wa
zamani kwa kuwapigia ndugu na jamaa pindi wanapougua hivyo ni vyema wakajiunga
na mfuko huo ilikupata msaada.
Singu amewataka watanzania kutambua kuwa Afya
ndio kila kitu na hawatoweza kuwa na afya bora kama hawana njia bora ya kupata
matibabu hivyo wanapokuwa na bima ya afya itawasaidia pindi wanapokuwa na
changamoto za kiafya.
‘Tupo hapa kwenye maadhimisho ya wiki ya
fedha kwa shughuli kubwa moja kuhudumia wananchi na kimsingi kuwapa elimu
kuhusiana na afya na elimu yetu hii inahusiana na fedha kwa sababu kama mtu
huna afya nzuri utajikuta unatumia fedha nyingi lakini ungekuwa umejiunga na
mfuko huo ungepata msaada’amesema Singu
Aidha Singu amesema kumekuwa na muako mkubwa
kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwani takwimu zinaonyesha kuna zaidi ya
watanzania Mill. 4 wanaohudumia na Bima ya Afya huku malengo lao yakiwa ni
kufika asilimia zaidi ya 50.
Hata hivyo Singu amesema kuwa mfuko huo umekuwa na mchango mkubwa katika uboreshaji wa huduma ambao umepelekea kupatikana na kwa huduma ambazo awali hazikutolewa ndani ya nchi.
Post a Comment